×

Msanii Maarufu wa Vichekesho, Zabogan Zabron Maarufu Kama Erick Amefariki Dunia

MSANII maarufu wa vichekesho, Zabogan Zabron maarufu kama Erick ‘Hivyo hivyo’ amefariki dunia.

Taarifa zilizothibitishwa na msanii mwenzake wa vichekesho, Tiny White, zinaeleza kuwa msanii huyo amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

Tiny White ameiambia Global Tv kwamba asubuhi ya leo alipigiwa simu na ndugu wa karibu wa Erick na kumpa taarifa za kifo chake.

Ameeleza kuwa Erick alikuwa mgonjwa ambapo hapo jana aliwasiliana naye na kumueleza kuwa alikuwa amevimba mwili mzima.

Erick amefariki dunia akiwa nyumbani kwao, Kibaha mkoani Pwani.

Leave a Comment