
Benki ya NBC yatangaza washindi wa “JAZA KIBUBU TUSEPE QATAR” siku ya Jumatano, Agosti 17, 2022. Ambapo kampeni hiyo ilianza Aprili mpaka mwezi wa September mwaka huu ikiwa na lengo la kutafuta washindi watakao hudhuria mechi za Kombe la Dunia linalotarajiwa kuanza mwezi Novemba mwaka huu, nchini Qatar.
“Washindi watakuwa ni wanne na Benki ya NBC itagharamia usafiri wa kutoka hapa kwenda Qatar, malazi na gharama zote zitakazohusika katika safari yote huko Qatar” Alisema.
Akiwataja washindi hao, ambao ni Bw. Abdallah Tangarisi (Singida), Victor George Mwaifunga (Dar es salaam), Konolia Leonard Hinju( Songea) na Mpoki Wamakimbika(Mbeya).Aliongeza kuwa, Washindi hawa wanatarajiwa kuondoka nchini mwezi Novemba mwaka huu, kuelekea nchini Qatar.