×

Watu Zaidi ya 16 Wafariki kwa Mafuriko China Kaskazini, Serikali Yaingilia Kati

Mafuriko, China Kaskazini

BEIJING Mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha huko jimbo la Qinghai kaskazini mwa nchi ya China yamesababisha vifo vya watu 16 huku wengine 36 wakiwa hawafahamiki walipo.

 

Mvua hiyo kubwa na ya ghafla ilianza kunyesha siku ya jumatano jioni maeneo ya milimani mwa jimbo hilo la Qinghai na hivyo kusababisha mmomonyoko wa ardhi na mikondo mikubwa ya maji kuelekea maeneo ya makazi ya watu.

Mvua kubwa imesababisha vifo vya watu zaidi ya 16 pamoja na kuharibu miundombinu

Mito ilifurika kwa maji na kubadilisha njia kuelekea maeneo ya vijiji na miji. Zaidi ya watu 6200 wameathiriwa na mafuriko hayo.

Jitihada za uokoaji zinaendelea

Serikali imefanya jitihada za uokoaji kwa kutuma timu ya watu zaidi ya 2000 na magari 160 kusaidia zoezi hilo la uokoaji.

 

Imeandikwa:  Simon J. Molanga kwa msaada wa mitandao

Leave a Comment