
MENEJA wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Kanda ya Dar es Salaam, Jonas Afumwisye Mwangunga, amefukuzwa kazi baada ya kudaiwa kupinga tozo na kumkashifu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kupitia group la WhatsApp, kinyume na kanuni za utumishi wa umma.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Masanja Kungu Kadogosa, imeeleza kuwa Mwangunga alipinga tozo kupitia miamala ya simu na miamala ya kibenki.

Alidai haoni faida ya ziara za Rais Samia nje ya nchi ikiwa wananchi wanaumizwa na tozo, na kudai Rais Samia anatumiwa na mabeberu. Afumwisye amefukuzwa kazi kwa mujibu wa sheria ya reli no.10 ya mwaka 2017 kifungu cha 13(f).
