Viongozi Mbalimbali Washiriki Sensa ya Watu na Makazi, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu…
Global Publishers August 23, 2022 0 Comments
SHARE THIS:
Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango pamoja na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakizungumza na Karani wa Sensa Isack Mgosho wakati walipokuwa wakihesabiwa katika Makazi yao Chanika Jijini Dar es salaam leo tarehe 23 Agosti 2022 kwenye Shughuli ya Sensa ya Watu na Makazi
VIONGOZI mbalimbali leo Jumanne, Agosti 23, 2022 wamekuwa miongoni mwa Watanzania waliohesabiwa katika Sensa ya Watu na Makazi.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akihojiwa na kutoa majibu ya dodoso kuu la Sensa ya Watu na Makazi kwa Karani wa Sensa Amina Mwambe wakati alipokuwa akihesabiwa katika Makazi yake ya Kijiji cha Nandagala, Ruangwa Mkoani Lindi Agosti 23, 2022.Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson ameshiriki zoezi la Sensa ya Watu na Makazi ambapo amehesabiwa katika makazi yake yaliyopo mtaa wa Sisimba, Uzunguni Jijini Mbeya.Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo akizungumza na Karani wa Sensa ya Watu na Makazi Bi. Faith Buruhani (kushoto) wakati wa kuhesabiwa kwenye makazi yake Msasani jijini Dar es salaam leo tarehe 23, Agosti 2022. (Picha na Adam H. Mzee/ CCM Makao Makuu)Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kulia) na mkewe Bi. Neema Mwigulu Lameck Nchemba, wakihesabiwa na Karani wa Sensa Bi. Rosemary Shani, katika zoezi la Sensa ya watu na Makazi, kijijini kwao Misigiri Kiomboi Iramba Mkoani Singida leo.