×

Kampuni ya Simu ya Infinix Yatoa Tv 11 kwa Washindi wa Promosheni ya Kali Kuliko

Kampuni ya simu Infinix kupitia promosheni ya kali kuliko ambayo imekua ikiendelea kwa kupindi chote hiki hadi Mwezi wa Septemba imetangaza rasmi washindi wa wiki ya pili wa promosheni ya Kali Kuliko ambapo TV 11 na Shopping Voucher zimetoka kwa washindi wa wiki hii.

Wateja ambao wamejishindia zawadi ya TV ni Fredrick Cosmas, Hidaya, Dayana, Maria na Kulwa kwa Mkoa wa Dar es Salaam, Mwanza Washindi ni Salma na Augustino, Mbeya Washindi ni Aloyce Sahawela na Anna Israel na Washindi wa kutoka Arusha ni Rechal na Rosemary.

 

Zawadi bado zitaendelea kutolewa kwa wateja wa wiki hii ya 3, kuanzia Tarehe 20 hadi Tarehe 26 ya Mwezi huu ukinunua Infinix NOTE 12 au HOT 12 series jina lako litaingia katika droo kubwa na Jumamosi ya Tarehe 27 washindi kutangazwa rasmi. Zawadi zitakazoshindaniwa ni DSTV decorder, Smart TV, Infinix Laptop au Infinix NOTE 12 VIP lakini pia unaweza Tembelea @infinixmobiletz kushiriki challenge ya #Kalikuliko2022 na ujishindie Infinix NOTE 12 VIP.

 

Japokuwa Infinix NOTE 12 na Infinix HOT 12 series ni simu za mwaka huu wa 2022 lakini kampuni ya simu Infinix imeamua kuwapendelea wateja wake waweze kunufaika na teknolojia mpya za smartphone kutoka katika kampuni hii uwezo wa chaji ya watt120 hutumia dakika 17 tu kujaa hadi asilimia 100%, kamera yenye uwezo wa kuchukua picha na video kwa quality nzuri pasipo kujalisha umbali wa kitu, tukio wala mazingira ya sehemu husika, Megapixel 108 za Infinix NOTE 12 zinauwezo mzuri wa kuleta uwiano wa rangi za picha.

 

CPU ya Mediatek G96 iliyopo katika simu hii ya Infinix NOTE 12 VIP inauwezo mkubwa wa kuendesha game ya aina zote pasipo kuzidiwa uwezo vile vile hufanya mawasiliano ya simu kati ya program moja kwenda nyengine kufanyika kwa haraka kutoka na kasi ya ufanisi katika simu mbali ya yote hii ni simu ya kwanza yenye sifa hizi ulimenguni kote kupatikana sokoni kwa bei ya sh.820,000 za Kitanzania.

KWA MASWALI ZAIDI PIGA NAMBA 0743558994

Leave a Comment