
MWANDISHI wa habari wa Mexico, Fredid Roman ameuawa kwa kupigigwa risasi na mwili wake kukutwa ukiwa ndani ya gari kwenye Jimbo la Guerrero lililopo Kusini mwa Mexico.
Hayo yamejiri muda mfupi baada ya mwandishi huyo kusambaza picha mitandaoni ya wanafunzi 43 walitoweka katika mazingira ya kutatanisha miaka nane iliyopita.
Tukio la wanafunzi hao lilitokea mwaka 2014 baada ya kuamuru basi kuelekea kwenye maandamano, linachukuliwa kuwa moja ya tukio baya zaidi kuwahi kutokea katika historia ya nchi hiyo.

Ofisi ya Mwendesha Mashtaka ya Mexico, imesema Roman ambaye anafanya kazi zake kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii na mwandishi wa Gazeti moja la Mexico walikutwa wamefariki ndani ya gari lililopo katika Mji wa Chilpancingo nchini humo.
Kwa mujibu wa rekodi za Shirika la Waandishi wa Habari Wasio na Mipaka (RSF), takwimu zinaonesha kuwa ndani ya mwaka huu waandishi wa habari 12 wameuawa nchini Mexico.
Pia, vyombo vingine vya habari nchini humo vimedai kuwa idadi ya waandishi wa habari waliouawa ni kati ya 15 au 16 tangu kuanza kwa mwaka 2022.
Imeandaliwa na Sanifa Khalifa kwa msaada wa mtandao