×

Saido Ntibazonkiza Aendelea Kushikiliwa Tanzania, Msemaji Atoa Tamko Zito

Saidi Ntibazonkiza akiwa na kikosi cha Timu ya Taifa ya Burundi

MCHEZAJI wa kimataifa wa Burundi ambaye msimu uliopita alikuwa akiitumikia klabu ya soka ya Yanga Saidi Ntibazonkiza anatarajiwa kurudi tena katika soka la Tanzania kufuatia kuhitajika na klabu ya ligi kuu ya Tanzania bara ya Geita Gold miezi michache baada ya kuachana na klabu ya Yanga.

 

Kupitia kituo cha Radio Msemaji wa klabu ya Geita Gold itakayoshiriki kwenye mashindano ya Shirikisho barani Afrika, amethibitisha klabu hiyo kumsajili Saido Ntibazonkiza na wakati wowote kuanzia sasa mchezaji huyo atajiunga na kikosi hicho cha Geita Gold ili kukiongezea nguvu kitakapokwenda kushindana kwenye mashindano ya shirikisho barani Afrika.

Saidi Ntibazonkiza

Ntibazonkiza aliachana na klabu ya Yanga kabla ya kuisha kwa msimu uliopita wa 2021/2022 sababu ikiwa ni kuisha kwa mkataba wake na klabu hiyo huku maneno ya chinichini yakisikika kuwa utovu wa nidhamu ni miongoni mwa sababu ya mchezaji huyo kuachwa kabla ya msimu kuisha.

 

 

Imeandikwa: Abdallah Kaputi kwa msaada wa mitandao.

Leave a Comment