
Baada ya Ukraine kufikisha miaka 31 ya uhuru tangu ilipojitoa kwenye utawala wa kisoviet, Katika siku ya uhuru Rais wa nchi hiyo Volodymyr Zelenskiy amewapongeza wananchi wa Ukraine na kuwataka kuzidi kupambana mpaka mwisho.
Siku kadhaa nyuma Rais Volodymyr Zelenskiy alionya kuhusu Urusi kufanya shambulio katika siku hiyo ya uhuru. Hii ni kutokana na Urusi kudai Ukraine imewaua wanajeshi wake katika mji wa Moscow.
Rais Volodymyr Zelenskiy alipokua akihutubia kupitia video alisema kua watu 22 wamekufa katika shambulio lililofanywa na Urusi huku likiacha watu wengine wakiwa majeruhi. Katika shambulio hilo lililofanywa kwa kutumia roketi liliharibu mabehewa manne na kuyaacha yakiungua moto.

Shambulio hilo limetokea katika mji mdogo wa Chaplyne kilomita zipatazo 145 kutoka mji wa Donetsk ambao umekaliwa na Urusi. Vita hivyo vimefikisha miezi sita tangu vilipoanza mwezi Februari mwaka huu.
Katika hali hiyo Rais wa Marekani Joe Biden amahidi kupeleka msaada wa kijeshi nchini Ukraine wenye thamani ya dola bilioni 3.
Imeandikwa:Dunstan Mtili Erick kwa msaada wa mitandao