
MLINZI wa klabu ya Leicester City raia wa Ufaransa Wesley Fofana anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake wa kujiunga na mabingwa mara mbili wa Ulaya Klabu ya Chelsea kwa ada inayokadiriwa kuwa zaidi ya paundi milioni 80 ambayo inamfanya kuwa beki ghali kuliko wote duniani.
Taarifa zilizoripotiwa na mitandao mbalimbali ya Habari ya Habari za michezo barani Ulaya zimebainisha kuwa klabu ya Chelsea pamoja na Leicester City zimekubaliana ada ya uhamisho ya paundi milioni 70 ambayo italipwa moja kwa moja na nyongeza ya zaidi ya paundi milioni 10 ambayo inatarajiwa kulipwa kulingana na makubaliano ya vipengele vya mkataba huo ili kumruhusu Fofana kujiunga na Chelsea.

Fofana (21) hakujumuishwa kwenye mchezo wa Ligi Kuu nchini Uingereza dhidi ya Southampton uliomalizika kwa Leicester Kupoteza kwa jumla ya mabao 3-2 huku pia mchezo wa mwisho wa wiki baina ya Chelsea nao pia hajajumuishwa kwenye kikosi.
Kama Chelsea itafanikiwa kukamilisha dili hilo la Fofana basi itahamishia nguvu zake katika kukamilisha dili la mshambuliaji raia wa Gabon Pierre Emerick Aubameyang, Anthony Gordon wa Everton pamoja na Kiungo wa Barcelona Frenkie De Jong