×

Maajabu ya Paji la Uso Wako, Zijue Siri za Imani za Kidini Zilizojificha Ndani Yake

 

Busu la paji la uso

WATAALAM wa mambo ya Imani wanasema kuna kitu ukiambiwa hutaamini kuhusu maajabu ya paji lako la uso.

 

Wanasema kuwa, paji la uso ndipo penye asili ya neno kipaji na hapo ndipo kuna lango la kuingilia mlango wa sita wa fahamu wa binadamu baada ya ile milango mitano ya mdomo, pua, macho, masikio na ngozi.

 

Wanaeleza kuwa, paji la uso ni jicho la ndani lisioonekana na ni lango kuu la kiroho.

Alama ya Sigda kwa Muislam

Kiimani katika Ukristo, kwenye ubatizo alama ya msalaba kwenye paji la uso ndiyo hukamilisha tendo na kuwa Mkristo kamili.

 

Pia wanasema kuwa, ukisoma Kitabu cha Ufunuo na habari za kutiwa Muhuri katika paji la uso utafahamu zaidi.

Alama ya msalaba kwa mkiristo ni ishara ya ukiristo kamili

Kwenye Uislam inafahamika nini maana na umuhimu wa swala tano na kuthibitisha uchaji wa Muislam katika swala tano ni sigida kwenye paji la uso.

 

Kwenye mapenzi busu la kwenye paji la uso ni tofauti kabisa na mabusu ya sehemu nyingine yoyote.

Cc; @sifaelpaul

Leave a Comment