
KOCHA MKUU wa Simba Zoran Maki amefurahia muuganiko wa safu ya ushambuliaji inayoongozwa na Clatous Chama, Augustine Okrah na Moses Phiri.
Kocha huyo amesema kuwa amefuhia kuona muunganiko mzuri wa washambuliaji hao, licha ya kutocheza kwa pamoja kwa muda mlefu lakini wana maelewano mazuri yaliyowawezesha kuiletea Simba ushindi katika michezo miwili iliyopita.

“Ni wachezaji ambao wameonesha kuwa na muunganiko mzuri na maelewano mazuri licha ya kutocheza kwa pamoja kwa muda mlefu ndani ya Simba , tayari unaona kila mmoja amefunga na kutengeneza nafasi nzuri na mimi ndilo jambo ninalolihitaji kutoka kwao kwa manufaa ya timu” amesema kocha huyo.
Okrah na Phiri wote ni wachezaji wapya ndani ya timu ya Simba, huku Chama akiwa mzoefu katika timu hiyo lakini wanacheza kwa maelewano makubwa jambo ambalo limewawezesha kuwaletea Simba ushindi mnono katika michezo miwili iliyopita.