×

Odinga Na Ruto Mpaka Kieleweke Kwenye Matokeo ya Uchaguzi, Mahakama Yaamuru Kura Kuhesabiwa Upya.

Raila Odinga

MAHAKAMA ya juu nchini Kenya imeamuru tume ya uchaguzi ya Kenya IEBC kumpa fursa mlalamikaji Bw.Raila Odinga Kuhakikisha data za uchaguzi kwenye kituo kikuu cha kuhesabiwa kura ambapo sava za system ya kupigia kura zipo.

 

Vilevile mahakama imeiamuru tume hiyo kumpatia masanduku ya vituo 15 ambavyo inahisiswa kura zake zilikua na kasoro kwenye kuhesabiwa.

 

Odinga amepewa mpaka alhamisi muda wa saa nane Mchana awe amewasilisha matokeo ya vituo hivyo ili kuicha mahakama kutoa maamuzi yaliyokua sahihi zaidi.

Raila Odinga akiwa na mgombea mwenzake

Wengine waliopewa ruhusa ya kuhakiki kura hizo ni aliyekua mgombea mwenza wa Odinga Bi. Martha Karua, na wengineo ambao ni Youth Advocacy for Africa (YAA), Peter Kirika, Khelef Khalifa, George Osewe, Ruth Mumbi na Grace Kamau.

 

Pia watapewa Habari zozote kuhusu utumiaji wa mfumo huo wa teknolojiana viwango vyake vya kuutumia, mazungumzo yaliofanyika ndani yake kwa utambulisho, ujumlishaji wa kura, utangazaji matokeo na uchapishaji matokeo hayo.

 

Imeandikwa:Dunstan Mtili Erick kwa msaada wa mitandao

Leave a Comment