×

Afghanistan Yasherehekea Uhuru Tangu Kuondoka kwa Majeshi ya Marekani

Mji wa Kabul uking’aa kwa taa za kupendeza

NI siku ya kuvutia katika mji wa Kabul nchini Afghanstan baada ya utawala wa Taliban kutangaza siku ya jumatano kua ni siku ya uhuru nchini humo.

 

Kabul ilipambwa na taa za kupendeza baada ya kutimia mwaka mmoja tangu majeshi ya marekani yalipoondoka na kuwaachia nchi yao.

 

Msemaji wa serikali Zabihullah Mujahid kupitia ujumbe wa twitter amesema kwamba ni Siku kuu ya Uhuru, wakati mamlaka zikifanya sherehe rasmi kwenye kituo cha jeshi la anga cha Bagram, ambacho kilitumiwa na vikosi wa Marekani kufanya mashambulizi ya anga dhidi ya Taliban.

Watu wa Afghanstan wakisheherekea Uhuru huo

Ingawa kuna sharia kali zaidi zilizowekwa na watawala wa Taliban zinawanyima wanawake hali ya kuishi Maisha ya kawaida. Pamoja na hayo yote watu wa nchini humo wamesema wanafurahia kuondoka kwa majeshi ya marekani waliosababisha waasi wa talibani kufanya machafuko kwa miaka 20 lakini sasa wanafurahia Maisha wanayoishi.

Imeandikwa:Dunstan Mtili Erick kwa msaada wa mitandao

Leave a Comment