
SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) zimetakiwa kushawishi na kuratibu Meli za kutoka Bandari za Congo, Zambia na Burundi kuanza kutia nanga katika Bandari ya Karema Wilayani Tanganyika Mkoa wa Katavi.
Wito huo umetolewa Septemba Mosi,2022 na Onesmo Buswelu (Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika) kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi. Mwanamvua Mrindoko,wakati aliposhuhudia Bandari hiyo ikianza kazi.
“Bandari iko tayari,TPA na TASAC popote mlipo hakikisheni mnaratibu Meli kubwa za kuja hapa wakati Serikali inatengeneza Meli ambazo zitakuwa za kisasa”
Bandari ya Karema iliyopo Wilayani Tanganyika Mkoa wa Katavi imeanza kazi kwa kushuhudiwa Boti ikishusha Abiria kutoka maeneo mbalimbali ya ukanda huo wa Ziwa Tanganyika ikiwa ni pamoja na Meli ndogo ya kitalii.

Kwa upande wao baadhi ya Abiria walioshuka katika Bandari hiyo wameeleza kufurahishwa kukamilika kwa Bandari hiyo kwani mwanzo maisha yao yalikuwa hatarini kutokana na kutokuwa na usafiri wa uhakika hasa wa Meli kubwa kutokana na kukosekana sehemu ya Meli kutia nanga.
Bandari ya Karema ilianza ujenzi wake Mwaka 2019 kwa ghalama ya Tsh. Bilioni 47.9 hivyo kuanza kutumika kunatajwa na Wafanyabiashara kama mkombozi wa Uchumi wao kwani wataweza kusafirisha Bidhaa zao kutoka Tanzania kwenda Nchi jirani za Congo,Zambia na Burundi bila wasi wasi.