×

Watu 4 Wauawa Katika Mapigano ya Makundi Yanayohasimiana Nchini Iraq 

Watu waliouawa

TAKRIBANI watu wanne wameuawa katika makabiliano kati ya wapiganaji wanaohasimiana yaliyotokea katika Mji wa Basra nchini Iraq huku makundi mbalimbali yakidaiwa kuhusika na tukio hilo.

 

Haya yamejiri baada ya kutokea machafuko ya mzozo wa kisiasa ambayo yanaendelea kushamiri katika mji huo hadi kufikia maeneo ya Kusini mwa nchi hiyo.

 

Maafisa wa Usalama wa Iraq wametoa taarifa hiyo na kueleza kuwa watu waliojihami kwa bunduki walivamia ofisi za serikali zilizopo katika Mji wa Basra zinazolindwa na vikosi vya usalama pamoja na jeshi linaloungwa mkono na Iran.

Maandamano Iraq

Maafisa hao hawakuweza kuwatambua watu waliojihami na kueleza wanaamini kwamba ni wafuasi wa kiongozi mwenye ushawishi mkubwa nchini humo aliyetangaza kujiondoa kwenye siasa anayefahamika kama Moqtada al-Sadr.

 

Kiongozi wa kundi moja la wanapiganaji wanayoungwa mkono na Iran, Qais al-Khazali ametoa amri ya kufungwa kwa ofisi zote za kundi lake na kuwaambia wafuasi wake wasilipize kisasi hata wataposhambuliwa.

Kiongozi aliyejitoa kwenye siasa, Muqtada Al Sadr

Nchi hiyo imekuwa ikikumbwa na mashambulio ya mara kwa mara na kusababisha vifo vya raia wa Iraq na majeruhi kadhaa pamoja na majengo kuharibika.

 

Imeandaliwa na Sanifa Khalifa kwa msaada wa mtandao

Leave a Comment