×

Klabu ya Coastal Union ya Tanga Yatambulisha Kocha Mkuu Mpya Raia wa Kenya

Katibu Mkuu wa Coastal Union, Omar A.S Ayoub (kushoto) ametambulisha kocha Yusuf Chipo ambaye amesaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuinoa timu hiyo.

Klabu ya Coastal Union ya Tanga imemtambulisha Kocha mkuu mpya, Yusuf Chipo raia wa Kenya kwa mkataba wa mwaka mmoja kukinoa kikosi hicho akichukua nafasi ya Juma Mgunda aliyejiunga na Simba Sc hivi Karibuni.

Kocha huyo amejiunga na Coastal Union akitokea Pamba FC ambapo Kabla ya Hapo alikuwa Kayanza FC inayoshiriki Ligi Kuu nchini Burundi.

MISHAHARA ya YANGA KUFURU, GSM Yafanya KWELI, HATMA ya Kocha MGUNDA Hii HAPA | KROSI DONGO..

Leave a Comment