Rais Samia: Kenya Imeonyesha Ukomavu wa Demokrasia kwa Nchi za Afrika Mashariki (Picha +Video)
Global Publishers September 13, 2022 0 Comments
SHARE THIS:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akihutubia viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wa Kenya katika Sherehe za Uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Kenya Dkt. William Samoei Ruto zilizofanyika kwenye uwanja wa Kasarani, Nairobi nchini Kenya tarehe 13 Septemba, 2022.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Septemba 13, 2022 amewapongeza wananchi wa Kenya kwa kuonyesha ukomavu wa demokrasia huku akisema wametoa zawadi pekee ya amani wakati wa uchaguzi kwa nchi nyingine za Afrika Mashariki.
Rais Samia ameeleza hayo jijini Nairobi wakati wa sherehe za kuapishwa kwa William Ruto kuwa Rais, ambaye alishinda uchaguzi mkuu uliofanyika Agosti 9 na kutangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC).
Rais Samia amesema wananchi wa Kenya wameonyesha ukomavu wa demokrasia Afrika Mashariki na kusisitiza kwamba sasa uchaguzi umekwisha, wasimame imara kuijenga nchi yao ya Kenya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akimpongeza Rais mpya wa Tano wa Jamhuri ya Kenya Dkt. William Samoei Ruto mara baada ya kuapishwa katika uwanja wa Kasarani Jijini Nairobi, tarehe 13 Septemba, 2022.Rais Samia akiwa pamoja na baadhi ya Marais wa nchi mbalimbali katika Sherehe za Uapisho zilizofanyika katika uwanja wa Kasarani Jijini Nairobi, nchini Kenya tarehe 13 Septemba, 2022.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiagana na Naibu Rais wa Jamhuri ya Kenya, Rigathi Gachagua mara baada ya Sherehe za Uapisho zilizofanyika katika uwanja wa Kasarani Jijini Nairobi, nchini Kenya tarehe 13 Septemba, 2022.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza na Baadhi ya Viongozi wa Serikali ya Kenya mara baada ya kumalizika Sherehe za Uapisho zilizofanyika katika uwanja wa Kasarani Jijini Nairobi, nchini Kenya tarehe 13 Septemba, 2022.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Kenya Dkt. William Samoei Ruto kabla ya uapisho Jijini Nairobi nchini Kenya tarehe 13 Septemba, 2022.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Kenya Dkt. William Samoei Ruto mara baada ya kuwasili Jijini Nairobi nchini Kenya tarehe 13 Septemba, 2022.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Jamhuri ya Kenya Dkt. William Samoei Ruto mara baada ya mazungumzo Nairobi nchini Kenya 13 Septemba, 2022.