×

William Ruto Aapishwa Kuwa Rais Kenya Katika Uwanja wa Kasarani, Nairobi – Video

Rais wa Kenya, William Ruto akiapishwa kuwa Rais wa Tano.

Dk William Ruto leo Septemba 13, 2022 ameapishwa kuwa Rais wa tano wa Jamhuri ya Kenya akichukua nafasi ya Uhuru Kenyatta ambaye amestaafu huku maelfu ya wananchi wakishangilia tukio hilo la kihistoria.

 

Sherehe za kumuapisha Ruto zimefanyika kwenye Uwanja wa Kasarani mjini Nairobi na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi, pamoja na viongozi wa nchi mbalimbali akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania.

 

William Ruto ameapishwa katika sherehe iliosimamiwa na msajili wa idara ya mahakama Anne Amadi na kushuhudiwa na jaji mkuu Martha Koome.

Mkewe Mama Rachel Ruto alikuwa amesimama kando yake wakati akila kiapo hicho.

“Mimi, William Samoei Ruto, kwa kutambua kikamilifu wito wa juu ninaochukua kama Rais wa Jamhuri ya Kenya, naapa kwamba nitakuwa mwaminifu wa kweli kwa Jamhuri ya Kenya, aliapa rais mpya William Ruto.

Wananchi wa kenya kwenye Uwanja wa Kasarani mjini Nairobi.

 

Martha Koome baadaye alimwalika rais anayeoondoka madarakani Uhuru Kenyatta, akiandamana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Kenya Jenerali Robert Kibochi kumkabidhi zana za mamlaka – Upanga wa Heshima na Katiba.

 

Na baadaye naibu wa rais Rigathi Gachagua pia naye alikula kiapo cha ofisi hiyo.

Baadaye bendera na picha ya rais anayeondoka mamlakani ilishukishwa huku bendera na picha ya rais mpya ikipandishwa, kabla ya mizinga ishirini na moja kupigwa ikiashiria utawala mpya.

Leave a Comment