×

Kigamboni Kuanza Msako Dhidi ya Panya Road, DC Atoa Tamko Zito

Panya Road

MKUU wa Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es salaam, Fatma Nyangasa jana alikutana na Wenyeviti wa Serikali za mitaa wa Wilaya hiyo katika mazungumzo yake aliwaonya vijana waliopanga kufanya uhalifu akisema polisi imeanza operesheni ya kukabiliana na vitendo hivyo.

 

Mkutano wa Nyangasa na Wenyeviti hao pamoja na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama uliofanyika jana Alhamisi Septemba 15, 2022 katika ofisi ya mkuu wa wilaya huyo, Nyangasa aliwahimiza wenyeviti hao kuhakikisha ulinzi shirikishi unafanyika kikamilifu na kutoa taarifa ya hali ya usalama katika maeneo yao.

 

“Kuanzia leo tumeanza operesheni maalumu katika maeneo na mitaa yote ya Kigamboni. Nyie (wenyeviti) ni viongozi kwenye mitaa kwa hiyo mtashiriki hili kikamilifu.

 

” Lengo ni kuhakikisha hakuna mtu mwenye nia au mipango ya kufanya  uhalifu kwa  Wanakigamboni, Jukumu letu ni kuwalinda wananchi wa Kigamboni  sote tuwajibike polisi wataingia mitaani na viongozi tushirikiane kwa kutoa taarifa sahihi,” amesema Nyangasa

Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kigamboni

Mkuu wa Polisi wilaya ya Kigamboni,(OCD) Thobias Walelo amesema timu yake ipo tayari kuhakikisha  ulinzi na usalama unaendelea kudumishwa wilayami humo huku akiwaonya vijana wasijihusishe katika vitendo vya uhalifu, pia aliongezea kuwa atakayekamatwa jeshi la polisi lipo tayari kumshughulikia pia aliwataka wananchi kutoa taarifa ili vitendo vya uhalifu vikomeshwe wilayani humo.

 

Imeandikwa na: Oswald Mwesiga kwa msaada wa mitandao.

Leave a Comment