×

Wanachama AAFP Wafurahia Sera Mpya Yenye Mrengo wa Kijinsia

Wanachama wakiwa kwenye mchakato wa kuandaa sera mpya wakiongozwa na Mwezeshaji wa Masuala ya Kijinsia kutoka TGNP, Iddi Mziray kushoto (mwenye kompyuta mpakato).

 

 

MTANDAO wa jinsia nchini, TGNP kwa kushirikiana na shirika la Kimataifa la WiLDAF umeendelea kutoa muongozo kwa vyama vya kisiasa hapa nchini katika kutunga sera mpya zenye mrengo wa kijinsia ili kila mtu aweze kunufaika na uwepo wa vyama hivyo.

Mwezeshaji wa Masuala ya Kijinsia kutoka TGNP, Iddi Mziray akiwa kwenye mchakato huo.

 

 

Miongoni mwa vyama vilivyonufaika na mpango huo ni chama cha siasa cha wakulima cha AAFP ambapo kiliongozwa na Mwezeshaji wa Masuala ya Kijinsia kutoka TGNP, Iddi Mziray.

 

Akizungumza na mwanahabari wetu Makamu Mwenyekiti wa Chama cha AAFP, Bara, Nansim Ndekaria ameishukuru TGNP na shirika la kimataifa la WiLDAF kwa kuwaamsha na kuwaelekeza umuhimu wa kuangalia sera yenye usawa wa kijinsia ndani ya chama chao na kusema kuwa sera hiyo itawaamsha wanawake na watu wenye uhitaji maalum katika kushiriki ipasavyo masuala ya siasa. Ambapo aliendelea kusema;

Makamu Mwenyekiti Bara wa Chama cha AAFP, Nansim Ndekaria akisikiliza kiumakini yaliyokuwa yakijadiliwa. 

 

 

“Kwa upande wangu naishukuru sana TGNP na WiLDAF kwa mpango wao huu wa kutusaidia kuandaa sera yenye usawa wa kijinsia.

Mimi nisema kumbe tulikuwa tumechelewa sana lakini wenzetu hawa ndiyo sasa wamekuja kutuamsha ambapo sera hii sasa itawafanya wanawake na watu wenye uhitaji maalum kushiriki kwa wingi masuala ya siasa tofauti na ilivyokuwa hapo awali.” Alimaliza kusema Makamu Mwenyekiti huyo.

Picha ya pamoja ya wanachama wa AAFP na Mwezeshaji wa Masuala ya Kijinsia kutoka TGNP, Iddi Mziray (katikati) baada ya mchakato huo uliofanyika ofisi za chama hicho zilizopo Tandika Bandari Dar.

 

Kwa upande wake Ndonge Saidi ambaye ni mlemavu wa ngozi (albino) amesema hapo awali sera ya chama hicho haikuwa na sehemu yeyote ya kuwaangalia walemavu lakini kwa sera hiyo mpya anaamini kuwa sasa nao wataanza kuangaliwa kiumakini zaidi tofauti na hapo awali.

 

Naye Mwezeshaji, Iddi Mziray kwa upande wake amesema amewashukuru sana washiriki wa kikao hicho kwa kuyaelewa vizuri aliyokuwa akiuwaelekeza ambapo nao walikuwa wakichangia mada vizuri kuonesha walipata ueleo wa kutosha maelekezo ya kitaalamu aliyokuwa akiwaelekeza.

HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS /GPL 

Leave a Comment