
ISRAEL itakuwa na balozi nchini Uturuki kwa mara ya kwanza baada ya miaka minne, ikiwa ni hatua ya hivi punde zaidi katika kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili kufuatia mpasuko wa miaka mingi.
Irit Lillian mwanadiplomasia mkuu ambaye amekuwa akisimamia ubalozi wa Israel mjini Ankara kwa miaka miwili iliyopita, atahudumu kama balozi wizara ya mambo ya nje ya Israel ilitangaza Jumatatu.

Mnamo mwaka wa 2018, Uturuki ilimuondoa balozi wake kutoka Israeli na kumwamuru balozi wa Israeli kuondoka akilalamikia mauaji ya Israeli ya makumi ya Wapalestina katika maandamano kwenye mpaka wa Gaza.
Uhusiano wa mara moja ulianza kuzorota baada ya kuchaguliwa kwa Recep Tayyip Erdogan, mkosoaji mkubwa wa jinsi Israeli inavyowatendea Wapalestina, kama waziri mkuu mwaka 2003.
Imeandikwa: leocardia Charles kwa msaada wa mitandao.