×

Waziri wa Afya Uganda Athibitisha Kuzuka Upya kwa Virusi vya Ebola

Maafisa wa afya wakijikinga dhidi ya Ebola

WAZIRI wa afya amewaambia waandishi wa habari kwamba mwathiriwa alikuwa ameonyesha dalili kabla ya kuugua ugonjwa huo.

 

Alikuwa mkazi wa kijiji cha Ngabano katika wilaya ya Mubende, yapata kilomita 147 (maili 91) kutoka mji mkuu, Kampala.

 

Kupitia Ujumbe waziri uliochapishwa kwenye ukurasa wa twitter wa wizara ya afya Uganda “Uganda yathibitisha kuzuka kwa Ugonjwa wa Virusi vya Ebola (EVD) katika Wilaya ya Mubende, Uganda.”

Tahadhari dhidi ya Ebola

Kisa kilichothibitishwa ni mwanamume mwenye umri wa miaka 24 mkazi wa kijiji cha Ngabano katika Kaunti Ndogo ya Madudu wilayani Mubende aliye na dalili za EVD na baadaye kufariki dunia.

 

Imeandikwa: Dunstan Mtili Erick kwa msaada wa mitndao

Leave a Comment