×

Mabondia Twaha Kiduku na Karim Mandonga Watua kwa Shangwe Mtwara Leo

Naibu Meya wa Manispaa ya Mikindani, Edward Kapwapwa wa kwanza kushoto, Twaha Kiduku, Mkuu wa Wilaya Mtwara, Dustan Kyobya na Karim Mandonga wakiongoza msafara wa kuelekea kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abasi Ahmed.

MABONDIA Twaha Kiduku na Karim Mandonga leo Septemba 21, 2022 wamepokewa kwa shangwe kubwa la wakazi wa Mtwara tayari kwa pambano la Ubabe Ubabe 2 huku wakikaribishwa na mkuu wa mkoa  Kanali  Ahmed Abasi Ahmed kwa kuwatakia ushindi mkubwa katika pambano la Jumamosi.

Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abasi Ahmed akiwa na mabondia Twaha Kiduku wa kwanza kushoto na Karim Mandonga baada ya kuwasili ofisini kwake.

Kiduku na Mandoga ambao mkoani hapa kwa usafari wa ndege walipokelewa na mkuu wa wilaya  ya Mtwara,  Dustan Kyobya akiwa na madiwani pamoja na wananchi walijitokeza katika mapokezi hayo kabla ya kufika kwa mkuu wa mkoa ambaye alitumia nafasi hiyo kuwakaribisha mabondia hao.

Bondia Twaha Kiduku akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya mkuu wa mkoa Mtwara akiwa na Karim Mandonga.

 

Pambano hilo ambalo limepangwa kufanyika katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona uliopo mkoani Mtwara chini ya udhamini wa Gazeti la Spoti Xtra, +255 Global Radio, Smart Gin, Creative Bee, Azam TV, Robby one pharmacy, H Fm, Swahili Water, Shujaa FM na Bongo Boxing Safari App huku kiingilio kikiwa ni Sh 5000 kawaida, Sh 10,000 VIP B na Sh 20,000 kwa VIP A.

Mabondia hao ambao walipitishwa katika mitaa mbalimbali ukiwemo katika mji mkongwe wa mikindani, soko kuu, chuo na stendi kuu ya mabasi Mkanaledi kabla ya kwenda kwa mkuu wa mkoa, Kanali Ahmed Abasi Ahmed ambaye aliwakaribisha mkoani hapa na kuwatakiwa ushindi kwenye pambano hilo la kimataifa huku akiwataka kutembelea vivutio vya kitalii vinavyopatikana mkoani hapa.

 

Kwa upande wa Kiduku na Mandonga wameshukuru mapokezi hayo pamoja na kamati  yote ya maandalizi ambapo kila mmoja ameahidi kutoa zaidi  ya ushindi siku ya Jumamosi.

Stori: Ibrahim Mussa

Leave a Comment