
Kwa mwaka wa pili mfululizo, Benki ya NMB imeshinda tuzo ya benki kiongozi wa kuwahudumia wateja binafsi nchini kutokana na ubora wa huduma zake kukidhi mahitaji ya huduma za kifedha za umma wa walio wengi.

NMB ilitunukiwa tuzo ya Benki Bora ya Wateja Binafsi Tanzania kwa mwaka 2022 kwenye hafla ya tuzo za Global Banking and Finance (GBAF) Awards zilizofanyika huko London, Uingereza.
Tuzo hizo zilianzishwa mwaka 2011 na jarida la Global Banking & Finance Review lenye wasomaji zaidi ya milioni tatu ulimwenguni kote na ambalo shughuli yake kubwa ni kuangazia matukio na maendeleo ya kifedha duniani.