×

Ofisa Habari Mpya Yanga Ally Kamwe Kimeeleweka Achukua Nafasi ya Bumbuli

KUTOKA KULIA: Msimamizi Mkuu wa Digitali na Maudhui wa Klabu ya Yanga (Digital Manager), Priva Abiud (Privaldinho),  Afisa Habari, Ally Kamwe Mkurugenzi wa Wanachama na Mashabiki ( Members and Fans Engagement), CPA Haji Mfikirwa wakiwa katika picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Andre Mtine (mwenye koti)

KLABU ya Yanga Septemba 27, 2022 imemtangaza Ally Kamwe kuwa Ofisa Habari mpya ameenda kuchukua nafasi ya Hassan Bumbuli ambaye mkataba wake uliisha Agosti mwaka huu.


Vilevile imemtambulisha pia Priva Abiud kuwa msimamizi mkuu wa Digitali na Maudhui.

Kamwe ni mchambuzi na mwandishi wa Habari za Michezo sawa na ilivyo kwa Privaldinho ambao wote ni familia ya waandishi wa Habari.

 

Pia Haji Mfikirwa yeye atakuwa kwenye kitengo cha fedha wakiwa pamoja na Mtendaji Mkuu wa Yanga.
Andrew Mtine ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Yanga naye ametambulishwa leo pia hivyo anaanza kazi na safu mpya kwenye idara ya habari.

 

Ni Haji Manara yeye ni Ofisa Habari wa Yanga lakini amekuwa kando kutokana na kufungiwa miaka miwili huku Hassan Bumbuli akiwa hajaongezewa mkataba baada ya kumaliza kandarasi yake Agosti.

CEO MPYA YANGA ATANGAZA VITA CAF, ALIKAMWE MAMBO SAFI YANGA KUANZA KAZI KWA KISHINDO…

Leave a Comment