×

Newcastle United Yafikia Makubaliano ya Usajili wa Mshambuliaji Kutoka Australia

Garang Kuol

KLABU ya Newcastle United ya nchini Uingereza imefikia makubaliano ya usajili wa kinda mwenye umri wa miaka 18 na mshambuliaji raia wa Australia Garang Kuol kutoka katika klabu ya Central Coast Mariners ambapo kinda huyo atajiunga na klabu yake mpya katika usajili wa dirisha dogo la mwezi Januari.

 

Taarifa zimebainisha kuwa Newcastle United imelipa kiasi cha Paundi 300,000 kama ada ya awali huku pesa nyingine ikiwekwa katika vipengele mbalimbali.

 

Akiongea mara baada ya kukamilisha dili hilo Kuol amesema:

 

“Siyo hali ya kawaida, kama kijana wa Australia Ligi Kuu ya Uingereza ni Ligi Kubwa ambayo kila mtu anaitazama lakini hakuna mtu anayehisi anaweza kufikia katika hatua hizo kuwa moja kati ya hao watu na kuwa kwenye nafasi ambayo nipo ni habari njema.” alisema Kuol.

Garang Kuol (18) atajiunga na Newcastle United mwezi Januari 2023

Kuol ambaye mwezi Juni alisaini mkataba wa kulipwa kwa mara ya kwanza alionesha kiwango kizuri katika michezo yake saba akiwa na klabu yake ambayo alifanikiwa kufunga jumla ya mabao 4 na michezo yote alikuwa akitokea benchi kiwango amabcho kimewashawishi mabosi wa Newcastle United na kukamlisha dili mapema kabla ya mwezi Januari.

 

 

 

 

 

Leave a Comment