×

Waziri wa Maji Azindua Bodi ya Sita ya Wakurugenzi wa Bonde la Wami/Ruvu

Waziri wa Maji Jumaa Aweso

WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso (Mb) Amezindua Bodi ya Sita ya Wakurugenzi Bonde la Wami/Ruvu na kuweka jiwe la Msingi la Jengo la Ofisi Mpya za Bodi hiyo ambapo Hafla ya Uzinduzi huo imefanyika Mkoani Morogoro.

 

Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mkoa, Kamati ya Siasa ya Mkoa, Kamati ya ulinzi na usalama, viongozi mbalimbali wa Dini, Menejimenti ya Bonde la Wami/ Ruvu Pamoja na Wadau mbalimbali wa Sekta ya Maji.

Ofisi mpya za Bodi

Katika Hafla hiyo Waziri Aweso ameitaka Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu kwenda kusimamia sheria ya usimamizi wa rasilimali za maji Kwa kuwashirikisha Wananchi kwa kuwapa elimu juu ya uhifadhi na utunzaji wa Vyanzo Vya Maji huku akibainisha kuwa Bonde la Wami/ Ruvu ndio liwe suluhisho la utatuzi wa changamoto za upatikani wa maji.

Waziri Aweso ametoa maagizo kukamilika haraka kwa Mradi wa Maji wa Mguru ndege

Aidha Waziri Aweso ametoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na usafi wa mazingira Morogoro (Moruwasa) kuhakikisha anakamilisha mradi wa mguru wa ndege utakao wezesha upatikani wa maji safi kwa Wananchi waishio maeneo ya kihonda mkoani Morogoro.

Leave a Comment