
Bwawa la ‘Nhwiga’ ( kiswahili lango la Twiga) lililopo kijiji cha Kizungwangoma kata ya Misheni wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza lenye historia ambalo ;ikitangazwa linaweza kuwa kivutio cha utalii wilayani Sengerema.
Bwawa hilo linalojaa maji wakati masika linahistori ya kuwa na njia kuu tatu za maji chini ya aridhi iyapeleka maji kwenye bwawa hilo pia linahistori ya matambiko ya kudaiwa kupotea kimiujiza kwa kila baada ya miaka kadhaa hususani wanapokwenda kuoga au kuvua samaki ndani ya bwawa hilo.
Katika kongamano la kutangaza vivutio vya utalii Kata ya misheni wilayani Sengerema mkoa mwanza Mashauri Joseph mkazi wa kijiji cha Kizugwangoma amesema bwawa hilo linahistoria ambayo haiwezi kufutika milele hivyo serikali kwa kushirikiana na jamii inapaswa kulitunza na kuwa kivutio cha utalii.
Kuitwa bwawa la Nhwiga (Kiswahil bwawa la Twiga) linahistori ya hapo zamani wakati wilayani Sengerema maeneo mengi yalikuwa poli wanyama aina ya Twiga kwa pamoja walikuwa wanakusanyika katika bwawa kunywa maji wakitokea maeneo mbalimbali.
Amesema hivi sasa bwawa hilo limepoteza dhana yake baada ya miti na na matete yaliyokuwa yakizunguka eneo hilo kukatwa baada ya maeneo hayo kwa sasa kuwa makazi ya watu.
Emanuel shimba mkazi wa kijiji cha Kizugwango amesema miaka ya 80 familia ya mojawapo ya maeneo hayo ilipoteza maisha kwenye bwawa hilo wakati ikioga lakini vifo hivyo vilitokana na matambiko.
Emmanuel Shimba ameongeza kuwa ipo haja serikali kwa kushirikiana na wananchi kulitangaza bwawa hilo ili liweze kuwa kivutio cha utalii na kuiwezesha serikali kupita fedha za kigeni.
Diwani wa kata ya Misheni Francis Mbungai amesema lengo la kufanya Kongamano la kutangaza vivuvitio vya utalii kata ya Misheni ilikuwa ni kutangaza bwawa hilo ambalo lina historia kubwa ambayo inapaswa kutangazwa na watu wafike ili kupata historia na kujionea vivutio vilivyopo.
Watanzania wametakiwa kutangaza vivutio vya utalii vilivyoko kwenye maeneo yao ili kuvutia watalii kifika kwenye maeneo yao