×

DCB Yaendelea Kung’ara Ikiadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja

Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya DCB, Bi. Zawadia Nanyaro (katikati) akikata keki huku wafanyakazi na wateja wa Benki ya tawi la Victoria wakishangilia, wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja, tawini hapo, Dar es Salaam wiki hii. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa.

Benki ya Biashara ya DCB imeendelea kung’ara wakati ikiadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa mwaka huu huku ikianisha baadhi ya mafanikio iliyopata tangu ilipoanzishwa Mwaka 2000.

 

-Benki ya kwanza kufuzu kutoka benki ya kijamii kwenda Benki ya Biashara.

 

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Godfrey Ndalahwa (kushoto) akikabidhi cheti cha shukurani kwa baadhi ya wajasiriamali ambao kituo chao kufanya vizuri kwenye mikopo ya vikundi inayotolewa na benki hiyo. Hii ilikuwa ni moja ya matukio kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja, jijini Dar es Salaam wiki hii. 
-Benki ya kwanza Tanzania kusajiliwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam.
-Benki inayoongozwa na watanzania kuanzia Bodi ya Wakurugenzi hadi Menejimenti.
-Benki imewanyanyua wajasiriamali wanawake zaidi ya 400,000 kupitia mikopo ya vikundi.
-Benki inatoa huduma na bidhaa zinazokidhi mahitaji ya wateja.
Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya DCB, Nelson Swai (katikati), akikabidhi msaada wa viti, mashine ya kuchapia (printa) na mifuniko ya tairi za gari vilivyotolewa na DCB kwa Mkuu wa Kituo cha Polisi  Magomeni, Mrakibu wa Polisi Edward Masunga, ikiwa ni sehemu ya matukio kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja, kituoni hapo, jijini Dar es Salaam.
-Benki ina Wateja kuanzia wajasiriamali wadogo, wafanyabiashara wa kati na wakubwa, wateja binafsi, waajiriwa, mashirika na makampuni.
-Benki ipo sambamba na waajiriwa na inatoa mikopo yenye riba nafuu.
-Benki ipo sambamba na wazazi kuwawezesha watoto elimu hadi chuo kikuu kupitia akaunti ya Skonga na mkopo wa ada.
-Benki inatoa mikopo ya nyumba yenye masharti nafuu.
-Fanya miamala na malipo mahali popote kupitia DCB Pesa, DCB Wakala, Visa, Master Card QR, DCB Malipo na Internet Banking.
-Kufanya miamala nje ya nchi kupitia International money transfer na Western Union.

Leave a Comment