
Dar es Salaam, 8th October – Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) na walaji wa vinywaji vikali wajumuika pamoja kuzindua kinywaji cha Captain Morgan Gold na kukiingiza sokoni rasmi jambo litakaloongezea chaguo la vinywaji vikali kwa wateja na biashara kwa bidhaa za SBL.

Uzinduzi huo wa SBL uliofanyika jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa The Waves, umeleta thamani katika biashara ya vinywaji vikali, kwa vile sasa kinatengenezwa ndani ya mipaka ya Tanzania tofauti na nyuma kilipokuwa kikitengenezwa nje ya nchi.
Mkuu wa Uvumbuzi wa SBL Bertha Vedastus, alisema kwamba kundi kubwa la walaji vijana na uchache wa bidhaa za vinywaji vikali ni kati ya sababu zilizowafanya wailete Captain Morgan Gold sokoni.
“Tafiti zinaonyesha kuwa walaji wetu makini vijana wanakosa machaguo ya kutosha ya vinywaji vikali, yanayoakisi mtindo wa maisha wanaoutaka na pia vinywaji vyenye ladha nzuri na vinavyopatikana kirahisi. Captain Morgan Gold inakuja kuwa chaguo bora kwao na kulipa soko nafasi nzuri ya kuuza bidhaa inayoakisi maisha ya watu, yenye mchanganyiko wa ladha nzuri na bei poa” alisema Bertha.
Mkuu wa Uvumbuzi aliongeza kwa kusema, “Bidhaa hii haiji sokoni kuongeza machaguo kwa walaji wetu makini nchi nzima, lakini pia kuongeza thamani katika sekta ya vinywaji kwa vile wajasiriamali watakuwa na chaguo la ziada lenye kufurahiwa na walaji kwa bei rahisi”.
Kinywaji hicho kikali, kinakuja sokoni kikiwa na historia ya utengenezaji yenye kusisimua na bei nzuri. Captain Morgan Gold itakuwa ikiuzwa kwa Tsh 5,000 kwa uzajo wa ml 200 na Tsh 20,000 kwa ml 750. Walaji wa Tanzania na wauzaji wa vinywaji vikali sasa wanajipatia nafasi ya kufurahia kinywaji chenye ubora wenye mchanganyiko wa matunda na ladha mbalimbali na zilizopikwa kwa umaridadi.
SBL inakuja kivingine katika soko la vinywaji vikali na kibunifu kushinda bidhaa zingine. Ili kufanya uzinduzi uwe wa kuvutia na maana, SBL iliwapa wateja taarifa juu ya vitu vilivyotumika kutengeneza kinywaji hicho na kuwapa walaji baadhi chupa zenye ujazo mbalimbali ili kujifurahisha na kujua ladha halisi.
Kinywaji hicho kikali kina mchanganyiko mzuri wa vanilla, sukari, matunda yaliyokaushwa na kiwango cha viungo vyenye mmea wa mwaloni, vyote vikiunganishwa kutengeneza kinywaji chenye ladha tamu. “Uzinduzi huu unatupeleka katika nafasi nzuri, ya kuwapa walaji wetu vinywaji vya kimataifa vyenye ladha yenye ubora kwa bei rahisi”aliongeza Bertha.
SBL inachukua hatamu za kuelekea kumiliki soko la vinywaji vikali kwa mara nyingine tena kwa kuongeza chaguo pendwa katika lundo la bidhaa zake nyingi. Uzinduzi huu unafuata nyanyo za Smirnoff, kinywaji kikali kilichofanya vizuri sokoni na barani kwa ujumla.