×

Mchezaji wa Brighton Raia wa Zambia Alazimika Kustaafu Soka kwa Matatizo ya Moyo

Kiungo Mkabaji wa klabu ya Brighton pamoja na timu ya taifa ya Zambia Enock Mwepu (24)

KIUNGO Mkabaji wa klabu ya Brighton and Hove Albion raia wa Zambia Enock Mwepu (24) amelazimika kustaafu soka kutokana na kukumbwa na matatizo ya moyo yaliyomkabili wakati akiwa kwenye ndege kujiunga na wenzake wa timu ya taifa ya Zambia akitokea klabuni kwake.

 

Taarifa iliyotolewa na klabu ya Brighton asubuhi ya leo imedai kuwa baada ya uchunguzi imebainika mchezaji huyo anaweza kupata shambulio la moyo kama ataendelea kucheza mpira wa miguu hivyo kitu pekee anachotakiwa kufanya ni kustaafu kucheza soka tu.

Enock Mwepu

Matatizo ya moyo kwa wachezaji limekuwa changamoto kubwa kwani kwa miaka ya hivi karibuni baadhi ya nyota kama Sergio Aguero pamoja na Christian Eriksen wamekumbana nayo huku Aguero akilazimika kustaafu soka mapema.

Leave a Comment