×

Wafanyakazi wa NMB Waanza Safari Kupanda Mlima Kilimanjaro

Ofisa Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) – Charles Ng’endo, akiwakabidhi rasmi bendera wafanyakazi wa Benki ya NMB watakayoipeperusha katika kilele cha Mlima Kilimanjaro. Akishuhudia ni Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini-Dismas Prosper (Mwenye  tisheti ya bluu).

Ikiwa ni mwendelezo wa kuadhimisha mwezi wa huduma kwa wateja, wafanyakazi 6 wa Benki ya NMB jana
wameanza safari ya siku 7 ya kupanda Mlima Kilimanjaro kupitia geti la Machame ambapo wataipeperusha
bendera ya benki hiyo katika kilele cha mlima huo.

 

Akizungumza katika hafla ya kuwaaga na kuwakabidhi rasmi bendera wafanyakazi hao, Ofisa Mkuu wa Hifadhi ya
Taifa ya Mlima Kilimanjaro(KINAPA),Charles Ng’endo alisema kama Hifadhi ya KINAPA wamefarijika sana na
utaratibu iliofanywa na NMB katika kuadhimisha mwezi huu muhimu wa huduma kwa wateja kwa kupanda Mlima
Kilimanjaro, aidha wao kama hifadhi watahakikishia kuwa wamewawekea mazingira mazuri na utaratibu mzuri wa
kuwahudumia mpaka wanafika kileleni.

Msafara wa wafanyakazi wa NMB wanaopanda Mlima Kilimanjaro wakiwa katika picha ya pamoja na wenzao wa Matawi ya Moshi, waliofika kuwatakia kila la kheri kabla ya safari yao ya siku 7.

Aliongeza kuwa “kufanya hivi kunatusaidia kutangaza utalii wa ndani na tunafahamu hifadhi ya Taifa TANAPA na
NMB tumekuwa na mahusiano ya karibu ya kibiashara na kiutoaji wa huduma kwa wananchi. Hivyo, kupanda
Mlima Kilimanjaro na kufika kileleni kutaimarisha mahusiano kati yetu sote na kupeleka ujumbe kwa wateja wetu
kuweza kutangaza utalii wa ndani.

 

Nae Meneja wa benki hiyo Kanda ya Kaskazini-Dismas Prosper alisema kuwa, NMB kwa kutambua umuhimu wa
sekta ya Utalii hapa nchini, waliona ni jambo la kifahari kusherekea mwezi wa huduma kwa wateja pamoja na
wateja wao ambao wapo katika hii kwa kupandamlima Kilimanjaro ili kuutangaza mlima huo. Timu hiyo
imepandishwa Mlima na kampuni ya Zara tours yenye uzoefu wa miaka mingi.

Msafara wa wafanyakazi wa NMB wanaopanda Mlima Kilimanjaro wakiwa wameanza safari yao ya siku 7.

Akimalizia kuzungumza, kiongozi wa msafara huo wa wafanyakazi wa NMB ambaye pia ni Afisa Mkuu wa Wateja
Wakubwa wa NMB, Alfred Shao alisema kuwa, NMB imefanya mambo mengi makubwa hapa nchini ikiwamo
kuwa Benki bora na yenye masuluhisho mengi ya kifedha kwa wateja wao na kwamba wanataka kuwadhihirishia
umma na wateja wao kuwa wanao uwezo wa kuwahudumia mpaka kilele cha Mlima Kilimanjaro na wajue
wanamaanisha wanaposema ‘NMB Karibu Yako’.

Wengine waliopanda Mlima ni Nishad Jinah, Stella Motto, Reginald Baynit, Agnes Mlolele na Christopher
Mwalugenge

Leave a Comment