
Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel Tanzania yasherehekea miaka 7 ya huduma kwa kuendelea kuwahakikishia wateja ubora na kasi ya mtandao wake kwa kuwapa huduma zenye ubunifu na kuendelea kuboresha huduma za mawasiliano hapa nchini.
Wakati ikifanya jitihada hizo, Halotel pia imekuwa ikibuni bidhaa mpya zenye lengo la kuwazawadia wateja wake na watanzania kwa ujumla wanaotumia huduma za mtandao mjini na vijijini.
Akiongea na waandishi wa Habari eneo la Mlimani City, Mkuu wa kitengo cha Bidhaa na Mawasiliano Halotel, Bi. Sakina Makabu amesema: "Leo kampuni ina habari njema kwa wateja wetu: tunazindua kampeni mpya kabambe kabisa inayojulikana kama “7 bang bang” kwa wateja wetu wote ambao wamekuwa wakituuunga mkono kwa kutumia huduma zetu toka tulipoanza na sasa tunatimiza miaka saba (07) ya utoaji huduma bora za mawasiliano hapa nchini.”

“Kampeni hii itawapa fursa wateja kushiriki katika Promosheni itakayowawezesha wateja wetu na wananchi wote kwa wale ambao watajiunga na mtandao wetu kushiriki katika bahati nasibu na kujishindia zawadi mbalimbali zikiwemo Vocha yenye thamani mpaka laki moja, Simu janja aina ya Samsung Galaxy A53 na A73, Televisheni janja 50’, Jokofu, Wifi router ya 4G na draw kubwa kabisa ya mwisho Gari Mpya aina ya IST ndani ya wiki 10.” Alisema Sakina,
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja Halotel, Bwa; Patrick Rwegoshora alisema Promosheni hii ni maalum kwa wateja wetu wote ikiwa ni moja ya ishara ya kuwashukuru kwa kuchagua na kutumia Mtandao wa Halotel.”

“Jinsi yakushiriki katika promosheni hii ni rahisi sana mteja wa Halotel anachotakiwa kufanya ni kuweka vocha zaidi kwenye laini yake, na moja kwa moja atakuwa katika nafasi ya kuingia kwenye droo ya bahati nasibu na kuweza kuibuka mshindi.
Hivyo kadri mteja anavyoweka vocha zaidi kwenye laini yake ndivyo anavyo jiwekea nafasi nzuri zaidi ya kushinda” aliongeza Patrick.
Halotel itatoa washindi 95 kila wiki, washindi 32 wa kila mwezi, washindi 16 kwa robo hii ya mwisho wa mwaka na mshindi moja wa mwisho wa promosheni (Grand draw) atajishindia Gari Mpyaa aina ya IST. Hivyo kutoa zawadi kwa jumla ya washindi 143 mpaka mwisho wa promosheni.
Pamoja na hayo mteja wa Halotel anaweza kutumia Huduma za HaloPesa katika kuingia kwenye droo ya ushindi kwa kununua vocha kupitia HaloPesa. Ikiwa pia ni njia rahisi na salama endapo mteja akiwa hana salio la kawaida.
Na katika muendelezo wa kusheherekea miaka ya huduma, HaloPesa inawaletea wateja promosheni ya Weekend ya tarehe 14/10/2022 mpaka 16/10/2022 bila Tozo. Ambapo mteja ataweza kufanya miamala kupitia HaloPesa App na atarudishiwa Tozo aliyokatwa. Aliongezea Afisa Masoko wa Halopesa Roxana Kadio.
Halotel tayari inatoa huduma ya kizazi cha nne cha huduma za mtandao wa 4G katika maeneo mengi ya nchi.