×

Tim Cook Afichua Sifa Nne za Kuajiriwa na Kufanya Kazi na Kampuni ya Apple

Tim Cook

MKURUGENZI Mkuu wa Kampuni ya Apple akiwepo katika chuo cha Naples Federico ll huko Italy awaambia wahitimu kuwa kampuni ya Apple inategemea utamaduni wao na nani ambao wanamuajiri, ikiwemo kuwa kampuni inatafuta wafanyakazi ambao wanasifa kuu nne.

 

Sifa ya kwanza ambayo Tim Cook ameongelea ni ushirikiano katika kazi ambapo anaamini kuwa sifa hio ya ushirikiano ni sababu ya nguvu ipelekeayo ubunifu wa vitu vipya katika kampuni yao ya Apple, kwa kampuni hio imeonekana kuwa ni mfumo mzuri kwa kuwa na ushirikiano baina ya wafanyakazi hii huepelekea kuwa na mazingira yaliyo bora katika eneo la kazi, Tim Cook amesema:

 

” Sio kama mtu anaenda kukaa kwenye kona au kabati na kuanza kugundua jinsi ya kutengeneza teknolojia yeye binafsi. ”

 

Katika maongezi yake na wahitimu katika chuo hicho, Tim Cook atamka sifa nyingine ambayo ni ubunifu wa hali ya juu, Cook amesema wanatafuta watu ambao wanafikiria tofauti kabisa na ikitokea tatizo sio mtu anatumia njia zile zile ambazo huwa zinatumika kutatua tatizo hilo bali kushughulisha akili na kutafuta njia mpya ya kutatua tatizo hilo.

 

Kuwa na shauku ya kutambua vitu tofauti tofauti, Kama mtoto mdogo ambavyo anakuwa anauliza maswali basi ndivyo mfanyakazi katika kampuni ya Apple anapaswa kuwa sababu mtu akiwa na tabia ya kutaka kujua itamjengea uzoefu wa kukumbana na matatizo magumu na atajua njia za kutatua tatizo hilo hivo hakuna maswali yanayoonekana bora Zaidi au yakijinga bali kila swali lina maana yake kuulizwa.

Tim Cook amesisitiza suala la ushirikiano kwa Wafanyakazi

Wafanyakazi katika Kampuni ya Apple pia wanapaswa kuwa na utaalamu kwenye kitu walichosomea shuleni ama uzoefu walioupata wakiwemo kazini, Tim Cook amesema:

 

“Kama tunafanya kitu katika kiwanda cha kufanya disaini, hivo tunahitaji mtu ambae ana ubunifu wa viwanda na ana ujuzi wa kutosha kutokana na shuleni alikosoma ama siku alizokuwa akifanya kazi.”

 

Ingawa Apple inahawahikikishia watu suala zima la kuwa na mazingira mazuri eneo la kufanyia kazi kwa mbinu ambazo wanatumia kuajiri wafanyakazi wao lakini kampuni hio imeacha mashaka kwenye vichwa vya watu kwa kuwa ilipokea alama “C” katika ukadiriaji wa mazingira ya kufanyia kazi katika makampuni yote kimataifa.

Leave a Comment