Rais Samia na Makamu wa Rais Washiriki Misa ya Kumuombea Baba wa Taifa Kagera
Global Publishers October 14, 2022 0 Comments
SHARE THIS:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais Mhe. Philip Isdor Mpango viongozi wengine wa Chama, Serikali, pamoja na Waumini wa Kanisa hilo wakiwa kwenye Misa Takatifu ya Kumuombea Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika Kanisa Kuu Katoliki, Jimbo la Bukoba Mkoani Kagera tarehe 14 Oktoba, 2022.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan pamoja na Makamu wa Rais, Philip Isdor Mpango leo Oktoba 14, 2022 wameshiriki Misa Takatifu ya kumuombea Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika Kanisa Kuu Katoliki, Jimbo la Bukoba Mkoani Kagera
Rais Samia akiwa kwenye picha na Makamu wa Rais, Philip Isdor Mpango , Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Bukoba Methodius Kilaini, Mapadri pamoja na viongozi mbalimbali mara baada ya Misa Takatifu ya Kumuombea Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.Rais Samia akisaini Kitabu cha Wageni Ofisini kwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Bukoba Methodius Kilaini mara baada ya Misa Takatifu ya Kumuombea Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika Kanisa Kuu Katoliki, Jimbo la Bukoba Mkoani Kagera tarehe 14 Oktoba, 2022