×

Muigizaji wa Filamu ya Moon Knight Aongea na Marvel Kuhusu Kurudi Kwake

Oscar Isaac, Muigizaji wa filamu ya MoonKnight

MSANII wa maigizo Oscar Isaac aliyechaguliwa kufanya katika filamu ya Moon Knight msimu wake wa kwanza kwa sasa yupo katika maongezi na kampuni ya kutengeneza sinema za mashujaa kuhusu kurudi kwake kwenye filamu hio kwa msimu wa pili, sinema zilizotengenzwa na kampuni hii kwa mwaka huu ni Thor: Love and Thunder, Black Panther na Doctor Strange in the Multiverse of Madness na zingine nyingi.

 

Hivi sasa bado haijawekwa wazi kama kutakuwa na msimu wa pili wa filamu ya Moon Knight lakini Isaac amesema kuwa hakuna taarifa zilizonyooka kuhusu kushiriki kwake katika filamu hiyo kwa msimu mwingine tena sababu hajui kama kutakuwa na muendelezo wa filamu ya Moon Knight.

 

Muigizaji huyo amesema kuwa hana upendeleo juu ya msimu wa pili ama kushirikiana na timu kubwa kama vile Midnight Suns, Isaac amesema:

Oscar Isaac akiwa katika kazi yake ya uigizaji

” Kiukweli, ni kuhusu hadithi. Kuna Hadithi yakusimuliwa? Je inavutia? Nitajihisi aibu pale ikishatoka? Kwahio ni kuhusu, kuna kitu cha thamani chakufanya umwage kila kitu  ulichonacho, na kwa Moon Knight hivyo ndivyo ilivokuwa.”

 

Isaac yuko tayari kucheza filamu katika aina yoyote ile ya umbizo ikiwa tu hadithi yake ni ya kusimuliwa, kwa maana hiyo Isaac yupo tayari kufanya maigizo ya filamu ya Moon Knight msimu wa pili ikiwa tu hadithi yake inavutia na ambayo itapendwa na watu kwa vile yeye anavutiwa zaidi na jinsi hadithi iinavyoweza kuburudisha na kuchangamsha watazamaji na yeye pia.

 

 

Imeandikwa na Arafat Ramadhan Salem kwa msaada wa mitandao

Leave a Comment