×

Sadio Mane Afunguka Kuhusu Maisha Yake, Awaasa Mastaa Duniani Kuijali Jamii

Raia wa Bambaly kijijini kwao na Sadio Mane wakiwa katika moja ya Hospitali zilizojengwa na nyota huyo

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Bayern Munich ya Nchini Ujerumani, raia wa Senegal Sadio Mane amefunguka na kuelezea vipaumbele vyake katika Maisha ya pamoja na soka kwa ujumla kuwa ni kwa ajili ya kurudisha kwa jamii.

 

Mane ambaye amefanikwa kuwa miongoni mwa wachezaji bora duniani akifanikiwa kumaliza katika nafasi ya pili ya mchezaji bora kwenye tuzo za Ballon D’ Or nyuma ya Karim Benzema amesema kuwa yeye hana haja wala nia ya kuishi Maisha ya kifahari ilihali watu wa jamii yake wanateseka na njaa.

 

Mane amenukuliwa akisema:

Sadio Mane akiwa na Rais wa Senegal Macky Sall

Sadio Mané : “Sijali sana kununua magari ya bei ghali au vifaa mahiri. Kipaumbele changu daima ni kuhakikisha watu wangu wa Senegal wanalala vitandani mwao na chakula, huduma bora za hospitali na shule.

 

“Sitapumzika hadi nifanye matokeo bora zaidi katika jamii yangu. Na nina furaha sana na ninajivunia wanasoka wengine ambao wanajiharibu kwa magari ya kifahari na nyumba, ni pesa zao, pia wanastahili kuzitumia kwa njia yao wenyewe.

 

“Kwa sasa nina mawazo yangu ya jinsi ya kutumia pesa yangu. Katika siku zijazo naweza pia kununua vitu vya anasa, lakini kwa sasa nataka kila mtu awe katika hali bora nyumbani.”

 

Sadio Mane amekuwa moja ya wachezaji wa kuigwa katika jamii ambapo kwa kiasi kikubwa ameisaidia jamii yake kwa kuwajengea Shule, Hospitali, Vituo vya mafuta pamoja na huduma mbalimbali za kijamii.

Leave a Comment