×

Uvccm Sengerema Wavuna Wanachama 50  Vyuo vya Ufundi

Picha ya pamoja  ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Sengerema, Patric Mundeba na wanachama 50 wapya.
Sengerema. Umoja wa Vijana wa chama Cha mapinduzi CCM wilaya ya Sengerema  imevuna wanachama 50 kutoka chuo cha maendeleo ya wananchi Sengerema (FDC) na kuwataka wanachama hao kuwa watiifua ndani ya umoja huo lengo nikukisaidia chama kuendelea kushika haramu.
Akizungumuza na waandishi wa habari leo Oktoba 24  mara ya baada ya hafla ya kupokea wanachama hao mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Sengerema Patric Mundeba amesema haya ni manufaa makubwa kwa umoja.
Amesema dhamila ya dhati ya umoja huo nikuhakikisha jumuiya hiyo inaimalika kwa kupata wanachama wapya ili kuendelea kuidumisha jumuiya hiyo ambayo ni msingi wa chama cha mapinduzi.
Amewapongeza  wabunge wa majimbo ya Sengerema, Hamis Tabasamu na Eric Shigongo wa Jimbo la Buchosa kwa kijitoa kwa dhati kusaidia jumuiya hiyo ili iweze kutekeleza majukumu yake.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Sengerema, Patric Mundeba
Mundeba amesema wabunge hao wamekuwa mstari wa mbele kuhakisha jumuiya hiyo inasimama katika misingi imara ndani ya chama cha Mapinduzi.
” Mimi kama mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana UVCCM wilaya ya Sengerema nitahakisha tunawaunganisha vijana kuwa wamoja ndani ya chama na nje ya chama , amesema Mundeba.
Mmoja wa Wanachama wapya Saimon John amesema kujiunga na chama cha mapinduzi kupitia jumuiya ya umoja wa Vijana UVCCM nimwanzo mzuri kwao kwa upanua uwigo wa mafanikio katika nyanja za kisiasa ndani ya chama hicho.
Katibu wa CCM wilaya ya Sengerema Muhusin Zikatimu amesema Jumuiya ya umoja wa vijina ndani ya CCM nitanuru la kupika viongozi  hivyo vijana hawa wametumia haki na maamuzi yao vizuri kujiunga na CCM.
” Mimi kama mtendaji mkuu katika Chama nitawapatia ushirikiano wa kutosha ili kutimiza malengo yao, amesema Zikatimu.
Jumuiya ya umoja wa Vijana wilayani Sengerema UVCCM wamewataka vijana kijitoa na kujituma ndani ya CCM ili Chama hicho kiendelee kushika dora.

Leave a Comment