Meneja wa Uhusiano na Elimu wa PSSSF,James Mlowe akizungumza wakati wa kikao kazi kilichofanyika kati ya mfuko huo na Chama Cha Waandishi wa habari(DCPC) jijini Dares Salaam.
MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), umewataka wastaafu wa mfuko huo kuwa makini na matapeli pindi wanapopata mafao yao.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kikao kazi kilichofanyika kati ya mfuko huo na Chama Cha Waandishi wa Habari Dar es Salaam DCPC, Meneja wa Uhusiano na Elimu wa PSSSF, James Mlowe amesema kuwa za wanachama wao hukumbwa na utapeli huo, kwasababu mbalimbali ikiwemo kutoa taarifa zao kwa wahusika wa wizi au matapeli kuwatumia maafisa waajili wa halmashauri mbalimbali kutafuta taarifa zao kwa njia za udanganyifu na wanapozipata hufanyia uhalifu huo.

“Hivi karibunii tuliwakamata matapeli watano, jijini Mwanza na tulipowahoji walisema huwatumia maofisa waajiri kupata taarifa zote za wastaafu ikiwemo waliajiriwa lini na namba zao za mishahara huku wakijifanya ni wafanyakazi kutoka Tamisemi na maafisa hao hutoa taarifa hizo wakiwa hawajui kwamba si mhusika hivyo tapeli anakuwa na kila kitu cha mstaafu na kisha kuwapigia simu kuwataka wapewe hela ili wapitishe michango mstaafu apate kumbe wanakuwa ni matapeli.”
“Hivyo niwaombe waandishi wa habari kusaidia kutoa elimu kwa wastaafu pindi anapopokea barua ya kustaafu anatakiwa kuanza hatua ya kufuatilia mafao yake, anatakiwa kwenda hatua inayofuata ya kufuata fomu ya PSSSF na kujaza ili kupeleka kwa mwajiri wake na sio kufanya mawasiliano na mfanyakazi yeyote wa PSSSF, ” amesema Mlowe.
Akizungumzia kuhusu mafanikio ya mfuko huo wa hifadhi ya jamii amesema kuwa mingozo inataka asilimia kumi ya makusanyo itumike lakini wao wameweza kutumia asilimia tano tu.
“Kama mwongozo unavyotaka tutumie asilimia kumi ya makusanyo lakini sisi tunatumia asilimia tano hivyo tunajitahidi kuendesha mfuko kwa ufanisi mkubwa ambapo watumishi laki moja na nusu wanalipwa kila mwezi tukitumia bilioni sitini na ikiwemo wastaafu, mafao ya uzazi na mafao mengineyo.
” Kuanzia mwaka jana tumeanzisha uhakiki kwa alama za vidole kwa kila mstaafu na kuweka divice katika wilaya zote na tunafanya michakato mpaka mwezi wa kumi na mbili kwa kila mstaafu atatakiwa kujihakiki kwa kutumia simu janja, “amesema.
Nae Mweyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Dar Es Salaam, Samson Kamalamo amesema kuwa kufuatia utapeli unaondelea watatumia kalamu zao kuelimisha jamii.
“Kama mlivyosema kumekuwa na utapeli kwa wastaafu hivyo basi tutawaelimisha wastaafu kwa kuwapa elimu pindi wanapostaafu kufuatilia mafao yao ni lazima wafike PSSSF kupata huduma na si kwa mtu mwingine,” alimaliza kusema. HABARI/PICHA NA MWANDISHI WETU /GPL