×

Waziri Mkuu wa Uingereza Sunak na Kitabu cha Utalii Tanzania

Rishi Sunak, Waziri Mkuu Mpywa wa Uingereza

WAZIRI MKUU mpya wa Uingereza, Rishi Sunak ameonekana katika picha akiwa ameshika kitabu cha utaliii kinachoeleza kuhusu masuala ya Wanyapori wa Tanzania na Muongozo wa Utalii.

 

Ikumbukwe kuwa, Sunak mzazi wake mmoja (mama yake) aitwaye Usha alizaliwa Shinyanga Mjini hapa nchini Tanzania (zamani Tanganyika) na kukulia huko na baba yake mzazi anayeitwa Yashvir amezaliwa nchini Kenya.

 

Wazazi wa Sunak mwenye umri wa miaka 42, wote wana asili ya India lakini baadaye waliondoka Afrika Mashariki na kuhamia nchini Uingereza miaka ya 1960.

Sunak aliyezaliwa Southampton ni msomi wa Chuo Kikuu cha Oxford na Stanford ambavyo ni vyuo vikuu bora duniani ndiye Waziri Mkuu mpya wa Uingereza akichukua nafasi ya Liz Truss aliyejiuzulu.

 

Hii ni mara ya Kwanza Uingereza katika Historia yake kupata Waziri mkuu asiye Mkristu.

 

Familia hiyo ina viongozi mbalimbali wakiwemo wabunge waandamamizi wa Chama cha Conservative, akiwemo Priti Patel, Braverman, Cleverly na Kwarteng, ambao wote walihamia Uingereza wakitokea Afrika Mashariki na Afrika Magharibi.

Leave a Comment