
Mchezo wa Ligi kuu ya NBC Tanzania bara kati ya Yanga na KMC uliopigwa kwenye dimba la Mkapa jijini Dar es salaam umemalizika kwa timu ya Yanga kuibuka na ushindi wa goli 1-0 ambapo Yanga anarudi na kujikita kileleni kwenye msimamo wa ligi kuu ya NBC akiwa na pointi 17.
Kutokana na ushindi huo, Yanga wanaendeleza rekodi yao ya kucheza michezo 44 ya ligi kuu Tanzania Bara bila ya kupoteza mchezo hata mmoja.

Aidha, licha ya Yanga kuweka rekodi hiyo, Kocha kutoka nchini Tunisia anaweka historia ya kuwa kocha ambaye ameiongoza Yanga kucheza michezo mingi zaidi kwenye ligi ya ndani hapa nchini Tanzania bila kupoteza mchezo hata mmoja, Nabi ametimiza michezo 44 ambayo ameiongoza Yanga kucheza bila kupoteza.