×

Wafanyakazi 9 Wa Davido Mbaroni Kifo cha Mwanaye

Msanii maarufu Barani Afrika Davido ambaye ameripotiwa kuondokewa na mtoto wake wa kiume aliyefariki baada ya kuzama kwenye bwawa la kuogelea (Swimming Pool)

WATU 9 akiwemo mpishi wa mtoto wa Staa wa muziki nchini Nigeria, #Davido na #Chioma aitwwye #Ifeanyi ambae amefariki dunia wakati akiogelea katika swimming pool ya nyumbani huko Lagos wanashikiliwa na Polisi katika Jimbo la Lagos kwa mahojiano kutokana na kifo cha mtoto huyo.

 

Mtoto wa taa huyo mkubwa Afrika #Ifeanyi (3) Alifariki katika swimming pool la nyumbani katika kisiwa cha Banana Lagos, jana Oktoba 31, 2022 na inasemekana wazazi wake #Davido na #Chioma hawakuwa nyumbani walikuwa kwenye ziara.

 

Kwa mujibu wa chanzo kimoja cha habari nchini Nigeria takriban watu tisa akiwemo mpishi wamekamatwa baada ya kifo cha mtoto huyo kutokana na uzembe uliofanyika mpaka mtoto akazama kwenye bwawa hilo.

 

Taarifa zaidi kuhusu msiba huo endelea kufuatilia www.globalpublishers.co.tz na mitandao yetu ya kijamii.

Leave a Comment