
KLABU ya Chelsea ya nchini Uingereza imeonesha nia ya dhati ya kuinasa Saini ya kinda wa Brazil kutoka katika klabu ya Palmeiras, Endrik huku ikikumbwa na upinzani mkubwa kutoka kwa klabu ya Real Madrid pamoja na Paris Saint Germain.
Endrik ambaye anacheza katika nafasi ya ushambuliaji akiwa na umri wa miaka 16 ameonesha kuwa moja ya vijana wenye kiwango cha hali ya juu ambacho kimemshawishi mmiliki mwenza wa klabu ya Chelsea Todd Boehly kumfungia kazi kinda huyo.

Baba wa kinda huyo Douglas ameibuka na kutoa kauli juu ya Sakata la kijana wake
“Hadi sasa hakuna chochote kilichoamuriwa na Real Madrid au klabu nyingine yoyote ile. Hatujapendelea hilo bado. Tutaamua katika kipindi cha miezi kadhaa ijayo kulingana na klabu ambayo italipa kiasi ambacho Palmeiras wanataka na watuoneshe Project nzuri kwa ajili ya Endrik. Watampata kijana.”
Kwenye mkataba wa Endrik una kipengele cha kiasi cha Euro milioni 60 kama klabu itataka kuvunja mkataba wake hviyo inasubiriwa kuona ni klabu gani itafanikiwa kuinasa Saini ya kinda huyo.