
Dar es Salaam: 11/11/2022. KAMPUNI ya Coca-Cola Kwanza kupitia kampeni yake ya Biriani Friday na Coka ambayo ilianza rasmi mwezi wa sita mwaka 2021 na kuendelea mpaka sasa ikiwa na lengo kubwa la kuendeleza utamaduni wetu wa Misosi na Coca cola ambapo huwa tunatembelea wadau wetu mbalimbali wanaojishughulisha na upikaji biriani kila Ijumaa kwa kuwaunga mkono na kuhakikisha tunawapatia wateja wao wote Coca-Cola ya baridi pale wapatapo Biriani kwenye migaha yao na kuwawezesha migahawa na vitendea kazi kama tshirts, Aprons na mikeka ya kutumia Biriani inapoliwa.
Kampeni yetu imeshafikia migahawa Zaidi ya50,kwa mikoa ya Dar-es salaam, Dodoma, Morogoro, Tanga, Mtwara, Zanzibar na Mbeya.

Kupitia Kampeni hii ya Biriani Friday na Coka tunaleta kwenu kwa mara nyingine tena Tamasha Kubwa la Biriani na Coka (BIRIANI FESTIVAL NA COKA) kwa wananchi wa Tanzania na hususani wa Makaao Makuu ya nchi DODOMA.
Ambapo tunawakutanisha kwa Pamoja wapishi wa Biriani wa mkoa huu na wateja wao, tamasha la mwaka huu litakuwa lakipekee kabisa na utofauti mkubwa, sababu tutaweza kupata Ladha pia ya vyakula vya asili vya Dodoma, Vionjo vingi vya kiasili ambavyo vinabeba utaifa wetu, na bila kusahau swala zima la kuangalia mechi za kombe la kimataifa ( World Cup), na tarehe hii kuna mechi nne nzuri na Kali.
Tutakuwa na Migahawa Zaidi ya 15, Michezo ya Watoto wetu, tukiburudishwa na Band yetu pendwa ya Bushoke na Dj mkali Dj D-ommy Pamoja na burudani nyengine nyingi, na zawadi mbali mbali.
Kupitia jukwaa hili napeda kuchukua nafasi hii kuwakaribisha watanzania wote, wapenzi na wadau wa biriani na Coca-Cola, Familia, Marafiki kuja kujionea na kushiriki kwenye utamaduni huu, Tanzania nchi yetu, Dodoma ndio makao makuu yetu, Biriani na Coca-Cola ndio chaguo letu na Mpira wa Kombe la dunia ndio raha yetu.
Tarehe ni 26/11/22 ( Jumamosi), Mahali ni viwanja vya wajenzi Maili Mbili Dodoma, kuanzia saa nne asubuhi.
Wahida Mbaraka- Meneja Biashara Na Masoko
Coca-Cola kwanza Ltd.