×

Raia wa Ukraine Wakusanyika Mitaani Kushangilia Kukombolewa kwa Kherson

Raia wa Ukraine wakiwa mtaani kusherehekea ushindi wa kukombolewa kwa Jimbo la Kherson

RAIA wa nchi ya Ukraine wameonekana kusherehekea ushindi wa majeshi yao baada ya kufanikiwa kukomboa Jimbo la Kherson kutoka kwenye mikono ya majeshi ya Urusi.

 

Vita kati ya Ukraine na Urusi bado inaendelea tangu ianze kwa mara ya kwanza Februari 24 mwaka huu huku kukiwa na wasiwasi huenda majeshi ya Urusi yakashindwa kuikamata nchi hiyo mara baada ya kuambulia anguko jingine kutokana na kukombolewa kwa jimbo la Kherson

 

Mwanzoni mwa vita hiyo Urusi ilishindwa kukamata Jimbo hata moja huku ikiambulia hasara kubwa kutokana na vifo vya askari wake pamoja na miundombinu lakini ilikuja kufanikiwa baadaye kukamata Majimbo ya Zaporinznzhia, Kherson, Donetsk pamoja na Luhansk lakini tayari Jimbo la Kherson limekuombolewa na wanajeshi wa Ukraine.

Raia wa Ukraine wakisherehekea ushindi majira ya usiku

Katibu Mkuu wa Ulinzi wa Uingereza Ben Wallace ameibuka na kudai kuwa kukombolewa kwa jimbo la Kherson kutoka kwa majeshi ya Urusi ni ishara nyingine kuwa Taifa hilo limefeli katika adhma yake ya kuishambulia Ukraine na hivyo ninpigo jingine kubwa kwa wafuasi watiifu wa Rais Vladimir Putin.

 

“Mwezi Februari Urusi ilishindwa kutimiza moja ya malengo yake makubwa isipokuwa kuikamata Kherson.

Sasa ikiwa tayari nalo limeshakombolewa watu wa kawaida sasa watakuwa wanajiuliza hii vita ilikuwa ya nini hasa?

Raia wa Ukraine

Walace amesema Urusi imeambulia hasara kubwa kutokana na vita yake haramu nchini Ukraine na mwisho wa siku imeambulia kutengwa na jumuiya za kimataifa pamoja na kudharirika.

 

Amemaliza kwa kuwahakikishia wananchi wa Ukraine kuwa Uingereza itaendelea kuisaidia Ukraine hadi ihakikishe vita inamalizika na Ukraine kuwa huru kama nchi nyingine.

Leave a Comment