Rais Samia Atunukiwa Shahada ya Udaktari wa Falsafa Katika Mahafali ya Chuo Kikuu cha Dar (Picha +Video)
Global Publishers November 30, 2022 0 Comments
SHARE THIS:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Wahitimu mbalimbali wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika Mahafali ya Hamsini na mbili (52) ya Duru ya Tano ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City tarehe 30, Novemba, 2022.
MKUU wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtunuku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Samia Suluhu Hassan Shahada ya Udaktari wa Falsafa wa Heshima katika Ukumbi wa Mlimani City.
Tukio hilo limetokea leo Novemba 30, 2022 alipokuwa ameshiriki mahafali ya 52 duru ya 5 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi pamoja na Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakati wa Mahafali ya Hamsini na mbili (52) ya Duru ya Tano ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City tarehe 30, Novemba, 2022.Rais Samia akitunukiwa Shahada ya Udaktari wa Falsafa wa Heshima ikiwa ni Shahada ya Udaktari wa Juu katika Humanitia na Sayansi Jamii na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika Mahafali ya Hamsini na mbili (52) ya Duru ya Tano ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City tarehe 30, Novemba, 2022.Rais Samia akikabidhiwa Cheti mara baada ya kutunukiwa Shahada ya Udaktari wa Falsafa wa Heshima ikiwa ni Shahada ya Udaktari wa Juu katika Humanitia na Sayansi Jamii na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.Rais Dkt. Samia akiwa kwenye picha ya pamoja Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kabla ya Mahafali.Rais Dkt. Samia akiwa na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa William Anangisye pamoja na Wahitimu wengine wakiwa kwenye Maandamano ya kuelekea ndani ya ukumbi wa Mlimani City kwa ajili ya Mahafali ya Hamsini na mbili (52) ya Duru ya Tano ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tarehe 30, Novemba, 2022.