
Uongozi wa klabu ya Geita Gold umethibitisha kuwa mkataba wake na kinara wa magoli Ligi kuu ya NBC msimu wa 2021/22, George Mpole umemalizika na kwamba makubaliano ya pande zote mbili yamefikiwa kuwa Mpole yupo huru kujiunga na klabu nyingine kuanzia leo Disemba 7 2022.
Geita Gold inamshukuru Mpole kwa kazi, ushirikiano na utendaji mzuri aliouonyesha kwa kipindi chote. Geita Gold inamtakia Mpole kila la kheri katika maisha yake ya mpira wa Miguu
