PM Majaliwa Akagua Ujenzi wa Hospitali ya Sumbawanga, Abaini Mapungufu
Global Publishers December 15, 2022 0 Comments
SHARE THIS:
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Mjini, Jacob Mtalitinya (wa pili kulia) wakati alipokagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Sumbawanga Mjini akiwa katika ziara ya Mkoa wa Rukwa, Disemba 15, 2022. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Queen Sendiga na kulia ni Kaimu Mhandisi wa Manispaa ya Sumbawanga, John Myovela. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua jengo la Kituo cha Afya Matanga ambalo alibaini kuwa limeanza kutumika wakati ujenzi haujakamilika katika baadhi ya maeneo. Alikuwa katika ziara ya Mkoa wa RukwaWaziri Mkuu Kassim Majaliwa akionesha maeneo ambayo bado hayajakamilika wakati alipokagua ujenzi wa Kituo cha Afya Matanga kilichopo katika Manispaa ya Sumbawanga ambacho kimeanza kutumika ingawa ujenzi haujakamilika katika baadhi ya maeneo. Alikuwa katika ziara ya kikazi ya Mkoa wa Rukwa, Disemba 15, 2022.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametembelea na kujionea maeneo ambayo bado hayajakamilika wakati alipokagua ujenzi wa Kituo cha Afya Matanga kilichopo katika Manispaa ya Sumbawanga ambacho kimeanza kutumika ingawa ujenzi wake bado haujakamilika katika baadhi ya maeneo ambapo amebaini baadhi ya mapungufu na kutoa mwongozo wa kutekeleza.