
Muuaji sugu wa Ufaransa anayejulikana kwa jina la Nyoka, aliyepatikana na hatia ya mauaji kadhaa ya watalii huko Asia katika miaka ya 1970, amerejea Ufaransa baada ya kuachiliwa kutoka gerezani huko Nepal.
Charles Sobrage mwenye umri wa miaka 78 aliachiliwa huru na uamuzi wa mahakama ambao ulizingatia umri wake na tabia yake nzuri.
Alifukuzwa na kurejeshwa nchini Ufaransa siku ya Ijumaa na kupigwa marufuku kurejea Nepal kwa takriban miaka 10.
Alikaa gerezani kwa miaka 19 huko Nepal kwa mauaji ya Wamarekani wawili mnamo 1975, ingawa hakufungwa kwa mauaji hayo hadi 2003.
Wakati huo huo, alihusishwa na mauaji zaidi ya 20 kati ya 1972 na 1982, wakati wahasiriwa walikuwa wakitiliwa dawa, kunyongwa, kupigwa au kuchomwa moto.
Wakati wa maisha yake, alikaa katika magereza katika nchi tofauti na angeweza kufanya uhalifu mwingi.